Uongozi wa FC Barcelona leo December 15 2016 wametangaza maamuzi waliyofikia na mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay anayeichezea timu hiyo Luis Suarez, Barcelona wamethibitisha kufikia makubaliano ya kumuongezea mkataba staa huyio.
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa dailymail.co.uk inaeleza kuwa Luis Suarez atasaini mkataba mpya utakaomuweka Nou Camp hadi mwaka 2021, makubaliano wamefikia na Ijumaa ya December 16 ndio atasaini rasmi mkataba.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na FC Barcelona mwaka 2014 akitokea timu ya Liverpool ya England kwa dau la pound milioni 75, Suarez kwa sasa akishirikiana na Lionel Messi na Neymar wamekuwa muhimili mkuu wa upatikanaji wa magoli wa timu ya FC Barcelona.
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0