Katika muendelezo wa kuwapatia wateja wake na watanzania wote kwa ujumla burudani za sikukuu, Vodacom Tanzania kwakushirikiana na wasanii wa WCB imeandaa matamasha mawili makubwa ambayo yatafanyika katika msimu huu wa sikukuu katika Mikoa ya Dar es Salaam na Iringa.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Nandi Mwiyomella alisema matamasha hayo makubwa ya muziki wa kizazi kipya yatafanyika katika mikoa ya Dar e salaam na Iringa chini ya wasanii Diamond Platinumz, Rayvanny, Rich Mavoko, Harmonize na Queen Darleen.
‘Kama mnavyoelewa msimu huu huwa umeambatana na shamrashamra mbalimbali za sikukuu na mitoko ukiwa na familia yako, Desember 24 kutashushwa show ya nguvu katika fukwe za Jangwani Sea Breeze Hotel ambapo kutakua na tamasha la kihistoria la Vodacom Wasafi Beach Party’;-Mwiyomella
‘Iringa tamasha litafanyika siku ya Krismasi katika uwanja wa Samora na matamasha yote yataanza saa nane mchana’;-Mwiyomella
Mwiyombella alisema burudani hiyo ya muziki ina kwenda sambamba na promosheni ya “NogeshaUpendo” http://vda.cm/nogeshaupendo ya Vodacom inayolenga kuwapatia wateja wote wa mtandao wa Vodacom zawadi za sikukuu ikiwa ni shukrani kwa wateja ambapo pia wateja wanayo fursa ya kujishindia tiketi za bure za kushiriki katika matamasha hayo makubwa katika msimu huu wa sikukuu.
‘Ili kujishindia tiketi ya bure anachotakiwa kufanya mteja wa Vodacom nikupiga*149*01# kisha nunua kifurushi chochote cha Vodacom na moja kwa moja utakua umeingia katika droo ya kuweza kujishindia tiketi. Zawadi nyingine kemkem kupitia promosheni ya NogeshaUpendo ni fedha taslimu, muda wa maongezi, Vifurushi vya interet’
Naye Diamond Platinumz aliongea kwa niaba ya wasanii wa WCB na kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Iringa kujitokeza kwa wingi siku ya show hizo kwani zitakuwa ni show za kihistoria katika mikoa hiyo miwili kufanywa na Vodacom kwa kushirikiana na WCB, amewawahakikishia mashabiki zake kwamba watakamuwa vilivyo akiwa na wasanii wenzake wote wa WCB kwa “KunogeshaUpendo”
VIDEO: Wakazi wa Dar na Iringa hii inakuhusu msimu huu wa sikukuu
VIDEO: Nogesha upendo na uwapendao ushinde zawadi Kemkem