Jana December 19 Ujerumani katika mji wa Berlin imeripotiwa kutokea shambulio lililopelekea mauaji ya watu kadhaa ikiwemo askari 9.
Taarifa nilizopata ni kuwa dakika 30 kabla ya kutokea kwa tukio hilo mtanzania Emily Mgeta anayecheza soka la kulipwa katika timu ya Freund Spiel Lauffen inayoshiriki Ligi daraja la tano nchini Ujerumani walipita eneo hilo akiwa na rafiki yake.
Ripota wa millardayo.com amefanikiwa kumpata katika exclusive interview Emily Mgeta akiwa Ujerumani aelezee kuhusiana na tukio hilo na hali ya usalama ilivyo kwa sasa Ujerumani katika mji wa Berlin.
“Ilikuwa jioni katika majira ya saa nilienda kumtembelea rafiki yangu Berlin, dakika 30 baadae rafiki yangua ananiambia pale tulipita kuna shambulio limefanyika na polisi 9 wameuwawa kiukweli imeniingia hofu imenibidi leo asubuhi na mapema nimwambie mimi narudi kule ninapokaa”
AUDIO: Mtanzania anayecheza Ujerumani ameeleza ubaguzi ulivyotaka kumkatisha tamaa