Usiku wa December 20 kuamkia December 21 kupitia mitandao mbalimbali ya soka imeandika kuhusiana na ombi la shirikisho la soka la Cameroon kwa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kuomba kuwafungiwa wachezaji ambao hawataki kucheza timu ya taifa.
Cameroon wameomba kufungiwa kwa wachezaji ambao hawataki kujumuika na timu ya taifa mwezi January na kucheza AFCON kwa ajili ya kuendelea kuvitumikia vilabu vyao, Cameroon imeomba FIFA kuwafungia wachezaji hao kucheza katika vilabu vyao wakati wote wa AFCON.
Imeripotiwa kuwa kuna list ya wachezaji 7 wa Cameroon ambao hawataki kujumuika na timu ya taifa January, Cameroon tayari imetaja list ya majina 35 ya wachezaji ambao wiki ijayo watachujwa hadi kufikia 23 ambao ndio watashiriki kucheza AFCON,
Staa wa Liverpool Joel Matip ni miongoni mwa wachezaji 7 waliogomea kuchezea Cameroon wakati wa AFCON mwezi January, wengine ni Andre Onana (Ajax Amsterdam), Guy N’dy Assembe (Nancy), Maxime Poundje (Girondins Bordeaux), Andre-Frank Zambo Anguissa (Olympique Marseille) Ibrahim Amadou (Lille), Alan Nyom (West Brom).
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3