Moja kati ya habari kubwa katika soka zilizoripotiwa usiku wa December 21 ni kuhusiana na mpango wa Man United kukaribia kukamilisha usajili wa beki wa kati wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Club Benfica ya Ureno Victor Lindelof.
Mitandao kadhaa ikiwemo The Sun imeripoti Man United wapo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Victor Lindelof kwa dau la pound milioni 42, Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira alienda England kukamilisha dili hilo, lakini inaripotiwa kuwa Victor atajiunga na Man United January.
Kama habari hizo zikiwa kweli na Victor Lindelof akawa kasajiliwa kwa pound milioni 42, atakuwa kavunja rekodi ya usajili ya Rio Ferdinand alipojiunga na Man United 2002 akitokea Leeds United kwa dau la pound milioni 29.1 na kuwa beki ghali zaidi katika historia ya Man United, rekodi ambayo itakuwa inavunjwa baada ya miaka 14.
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3