Jumanne ya December 27 2016 timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilishuka uwanjani kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Ubelgiji katika uwanja wake wa Luminus Arena dhidi ya KAA Gent ikiwa chini ya kocha wao msaidizi.
KRC Genk ambao kwa sasa wataanza kufundishwa na kocha msaidizi wa zamani wa Man United Albert Stuivenberg, wamefanikiwa kuwafunga KAA Gent kwa jumla ya goli 2-0, magoli yakifungwa na Aljandro Pozuelo dakika ya 19 na Nikolaos Karelis kwa mkwaju wa penati dakika ya 25.
Kwa upande wa mtanzania Mbwana Samatta yeye aliingia dakika ya 51 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis aliyeshindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia, katika michezo yao mitano iliyopita KRC Genk alikuwa hajamfunga KAA Gent hata mechi moja wakiwa wamefungwa mechi nne na kutoka sare mechi 1.
KRC Genk bado wapo nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji, wamefikisha jumla ya point 28. pic.twitter.com/Iw8OjxmM5N
— millard ayo (@millardayo) December 27, 2016
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3