Zikiwa zimesalia siku chache tu ili Rais wa Marekani Barack Obama amkabidhi madaraka ya uongozi wa nchi mrithi wake Donald Trump aliyeshinda uchaguzi wa urais wa mwaka jana. Barack Obama amechukua uamuzi wa kubatilisha kifungo alichohukumiwa Chelsea Manning, aliyekuwa mwanajeshi wa Marekani ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kufichua nyaraka za siri.
Mwanajeshi huyo aliyekuwa mwanamageuzi aliyefanya kazi nchini Iraq alikuwa akijulikana pia kama Bradley Manning alikutwa na hatia ya kufichua nyaraka za siri mwaka 2013 kwa kuweka karibia robo tatu ya mamilioni ya nyaraka za siri za kijeshi na kidiplomasia katika tovuti ya WikiLeaks.
Taarifa kutoka Ikulu zinasema Manning ataachiwa huru ifikapo mwezi wa tano. Rais Obama pia ametoa msamaha kwa aliye kuwa afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Marekani Jenerali James Cartwright, aliyekubali kosa la kutoa taarifa za uongo katika uchunguzi uliokuwa ukifanywa na FBI katika udukuzi wa compyuta kuhusu mipango ya kinyuklia ya Iran.
VIDEO: Wafanyabiashara Arusha wakataa kuondoka kwenye maduka, Meya azungumzia hilo, Bonyeza play hapa chini