Baada ya kuchezwa michezo ya kwanza ya Kundi A siku ya ufunguzi wa michuano ya mataifa ya Afrika 2017 January 14 katika uwanja wa Stade de Amitie Libreville na timu zote nne kumaliza michezo yao ya kwanza kwa kufungana sare ya 1-1, Jumatano ya January 18 ilikuwa siku ya michezo ya pili ya kundi hilo.
Mchezo wa kwanza kwa siku ya January 18 2017 ulikuwa ni mchezo kati ya Gabon dhidi ya Burkinafaso ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1, Cameroon wakaingia uwanjani kucheza dhidi ya Guinea Bissau na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 na kuwafanya wao wa ndio wawe timu ya kwanza kupata ushindi katika timu za Kundi A.
Magoli ya Cameroon yalifungwa na Sebastien Siani na Michael Ngadeu huku goli pekee la Guinea Bissau lilifungwa na Piqueti Brito Silva., ushindi huo umeifanya Cameroon ipate nafasi ya kuongoza Kundi A kwa kuwa na point nne, huku Guinea Bissau ikishika mkiwa kwa kuwa na point moja.
https://youtu.be/F2l-YK_Lpig
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4