Tumekuwa tukisikia stori za treni zenye kasi kuzinduliwa maeneo mbalimbali duniani kama vile China, sasa taarifa iliyotolewa leo January 20 2017 imeeleza kuwa treni ya kwanza na yenye kasi zaidi Afrika itaanza kutumika Morocco.
Unaambiwa treni hiyo ina uwezo wa kuzimaliza kilometa 321 kwa saa ambapo kwa harakaharaka ingekua Tanzania inaweza kufika Arusha ikitokea Dar kwa dakika zisizofika 120.
Pesa iliyotumika kwenye huu mradi ni Dola za kimarekani BILIONI 2, ni pesa ndefu ambayo imepatikana baada ya mradi huo kuwekewa mikono na nchi 6, serikali ya Morocco yenyewe, Ufaransa, Saudi Arabia, Kuwait, na UAE.
ULIPITWA? Tazama kwenye hii video hapa chini kuona mradi wa nyumba 1500 zinazojengwa Kigamboni Dar es salaam na Mtanzania, watu wataishi kwenye eneo lililozungushiwa uzio na ulinzi mkali ndani ya kijiji kimoja.