Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika timu ya taifa ya Ivory Coast usiku wa January 24 ndio siku rasmi ilivuliwa ubingwa wa mataifa ya Afrika, baada ya kuruhusu kufungwa goli 1-0 na timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi C.
Ivory Coast ambao walikuwa Kundi C na timu za Morocco, Togo na DR Congo, wamejikuta wakifungwa goli 1-0 na kushindwa kusawazisha, Ivory Coast wameondolewa katika michuano hiyo kwa kumaliza nafasi ya tatu na kama wangepata ushindi leo dhidi ya Morocco wangefuzu kucheza robo fainali.
Kocha wa Morocco Herve Renard ambaye kawavua Ubingwa Ivory Coast, ndio kocha aliyewapata taji hilo Ivory Coast mwaka 2015 akiwa anaifundisha timu hiyo, Rachid Alioui ndio alihitimisha safari ya Ivory Coast kwa goli alilofunga dakika ya 64.
https://youtu.be/EVGkdB7jDJU
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4