Wawakilishi pekee wa ukanda wa Afrika Mashariki katika michuano ya mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 timu ya taifa ya Uganda, usiku wa January 25 walicheza mchezo wao wa mwisho wa kukamilisha ratiba ya michuano ya AFCON 2017 dhidi ya Mali.
Uganda wamecheza mchezo huo wa kukamilisha ratiba lakini tayari walikuwa washatolewa katika michuano hiyo, Uganda wamelazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 lakini wameweka rekodi ya kufunga goli lao la kwanza la AFCON toka washiriki michuano ya AFCON kwa mara ya mwisho 1978.
Goli la Uganda lililofungwa na Farouk Miya dakika ya 70, limefungwa baada ya miaka 39 toka timu hiyo ishiriki AFCON, lakini Yves Bissouma aliisawazishia Mali dakika ya 73 na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya 1-1 na Uganda kurudi nyumbani wakiwa wameambulia point moja na kuziacha Ghana na Misri zikisonga mbele.
https://youtu.be/EfIQ9Hsa6SA
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4