Shikisho la soka Tanzania TFF leo February 6 2017 ilitangaza ratiba ya hatua ya 16 bora ya Kombe la shirikisho ambalo maarufu kama Azam Sports Federation Cup, ratiba hiyo imepangwa lakini baada ya kutoka watu wengi katika mitandao wakataka kufahamu vigezo ilivyotumika kupangwa kwa ratiba hiyo.
Kwani kuna baadhi ya timu kama Simba na Yanga inaonekana kupangiwa na timu zinazodhaniwa kuwa nyepesi wakati Azam FC akipangiwa Mtibwa Sugar, Ayo TV imempata afisa habari wa TFF Alfred Lucas kuzungumzia vigezo vilivyotumika kupanga ratiba hiyo.
“Vigezo vilivyotumika kwa kanuni zetu sisi, vimetumika vitatu cha kwanza kabisa performance ya hizi timu na wapinzani wao, lakini pili tumeangalia geographia ya timu inapotoka kuendana na ratiba ya Ligi, mwisho ni kuzipunguzia gharama ya timu kusafiri” >>>Alfred Lucas
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4