Usiku wa February 5 2017 timu ya taifa ya Cameroon ilichukua taji lake la 5 la AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Misri kwa kuifunga kwa goli 2-1, Cameroon walitwaa taji hilo ikiwa ni miaka 15 imepita toka kikosi chao kitwae taji hilo kwa mara ya mwisho.
Baada ya ushindi huo kocha wa Cameroon Hugo Broos aliongea na vyombo vya habari na kugusia kuhusiana na wale mastaa nane wa Cameroon waliyogoma kujiunga na timu kwa ajili ya kuendelea kuvitumikia vilabu vyao akiwemo staa wa Liverpool Joel Matip.
“Kulikuwa na tatizo hapo awali kuhusiana na wachezaji ambao waligoma kuungana na sisi, huwezi kuwalaumu ni maamuzi yao lakini sasa hivi labda wanajilaumu kwa nini hawakuja AFCON, tulikuja hapa nafikiri kulikuwa hakuna mtu aliyefikiria kama tutafika mbali”
“Nilikuja hapa nikiwa na marafiki 23 sio wachezaji 23 tumekaa pamoja kwa wiki kadhaa tukabadilika kutoka kuwa timu na kuwa wanafamilia, hii ndio ilikuwa sababu ya kutwaa Ubingwa lakini hakuna aliyeamini walichokifanya wachezaji”
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4