February 9 2017 Wabunge walikuwa wakichangia maoni kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya ardhi, maliasili na utalii pamoja na kamati ya Kilimo, mifugo na maji.
Kati ya waliuopata nafasi ya kusimama ni Mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa yeye aliguswa na kuendelea kwa matukio ya mauji ya wakulima na wafugaji yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo jimboni kwake Rufiji.
‘Nimesikitishwa sana na taarifa hii ya kamati ambayo imeshindwa kuomna kuwa mgogoro wa wakulima na wafugaji ni mkubwa ambao unahitaji serikali kuingili akati na haraka, hiki ni kilio cha wakulima wote nchini lakini iweje serikali ishindwe kuutatua‘ -Mohamed Mchengerwa
‘Amani ya nchi tuliyoachiwa na baba wa taifa inakwenda kupotea kwasababu ya wakulima na wafugaji, nimelisema hili wa muda mrefu sana na naambo bunge litambue kuwa Rufiji hatuna mgogoro wa ardhi bali mwingiliano wa jinai unaofanywa na wafugaji katika maeneo ya wakulima‘ -Mohamed Mchengerwa
‘Tatizo hili ni kubwa na mwezi wa kumi na moja watu wawili wameuawa kwa mkulima alichinjwa na mfugaji alichomwa moto akiwa hai lakini ajabu hakuna kiongozi wa serikali jata mmoja alifika katika maeneo husika ili kuweza kuondoa mgogoro huu mkubwa‘ -Mohamed Mchengerwa
Unaweza kuendelea kumsikiliza Mbunge Mchengerwa kwenye hii video hapa chini……
BUNGENI: Maswali na majibu ya February 9 2017