Kila nchi duniani imekuwa na utaratibu wake na hata zingine kupiga marufuku baadhi ya vitu kulingana na utamaduni wa nchi husika, Leo nimekutana na hizi nchi 10 ambazo zimepiga marufuku vitu ambavyo vinashangaza zaidi.
10. Ugiriki – Video Games.
Serikali ya Ugiriki imepiga marufuku video games nchini kote tangu mwaka 2002 na anayekiuka anakwenda jela.
9. Malaysia – Nguo za Njano
Uvaaji nguo zenye rangi ya njano au kitu chochote chenye rangi ya njano kama kiatu ni kinyume cha sheria nchini Malaysia kwa kuwa rangi ya njano nchini humo huchukuliwa kama ‘rangi ya waandamanaji’.
8. Denmark – Kumpa mtoto Jina
Serikali ya Denmark imeweka sheria kwa wazazi kuwapa majina watoto wao, unaweza kuchagua majina kwenye orodha ya majina 24,000 iliyotolewa, kama utahitaji kumpa jina mtoto wako utahitaji kupata ruhusa rasmi kutoka serikalini.
7. Iran
Serikali ya Iran imeamua kupiga marufuku mambo kadhaa ya magharibi kama vile muziki wa magharibi, Skinny Jeans, tattoo, kunyoa style ya nywele za magharibi imepigwa marufuku kwa kile walichodai style za magharibi ni ishara ya kuabudu shetani.
6. China – Ua la Jasmine
Baada ya mapinduzi ya Tunisia’s Jasmine, utawala wa kichina ulipiga marufuku uuzwaji wa ua la Jasmine, watu hawaruhusiwi kuuza na hata kulizungumzia ua hilo China kwa kile walichodai Jasmine ina nafasi kubwa kudhoofisha demokrasia ya nchi hiyo.
5. Burundi – Jogging
Unaambiwa nchini Burundi ukifanya jogging nyakati za asubuhi na mapema itakupelekea kufungwa jela. Inaeelezwa kuwa Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza, alipiga marufuku ili kukomesha migogoro kati ya makundi ya kikabila nchini humo.
4. Ufaransa – Kutumia tomato
Nchini Ufaransa wanafunzi wa nchi hiyo wamepigwa marufuku kutumia tomato kwenye chakula, hasa kwenye hoteli za shule mbalimbali baada ya Serikali kugundua kuwa vijana wanatumia zaidi.
3. Australia – Cinema za ngono
Nchini Australia unaambiwa kuigiza sinema za ngono sio kosa la jinai kitu cha kushangaza ni kwamba sinema ya ngono inayomshirikisha mwanamke mwenye matiti madogo zimepigwa marufuku.
2. Saudi Arabia – Wanawake kuzurura
Saudi Arabia inaelezwa kuwa taifa kali zaidi duniani linapokuja suala la wanawake, kuna vingi vimepigwa marufuku kuhusu wanawake. Nchi hii imepiga marufuku kwa wanawake kuendesha gari, wanawake kuzurura, Serikali ya nchi hiyo inasimamia sheria kwenye maeneo mbalimbali kuzuia jinsia tofauti kuwa pamoja hadharani isipokuwa wanandoa.
1. Korea Kaskazini – Jina la Korea Kaskazini
Watu wa Korea Kaskazini hawaruhusiwi kuangalia TV, kucheza muziki, kuondoka nchini, kutoa maoni yao, kucheka hadharani, kuamini katika dini, kuvaa jeans ya blue, kingine ni kwamba ni kosa kuita Korea Kaskazini nchini Korea Kaskazini inabidi uite ‘Korea’ kama aitafanyika hivyo jiandae kwenda jela.
AyoTVMAGAZETI: Lema atikisa, Kilichomponza Gwajima polisi, Bonyeza play hapa chini kutazama