Timu ya Yanga ambayo ni Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara watasafiri asubuhi ya February 11 2017 kuelekea Moron Comoro ikiwa ni siku moja tu kabla ya kucheza game yao ya round ya kwanza wa klabu Bingwa Afrika vs Ngaya Dembe.
Tumezoea kuona timu zinasafiri mapema kwenda sehemu itakapochezwa mechi na wapinzani wao ili wazoee hali ya hewa lakini kwa nini Yanga wamechelewa? kocha msaidizi wa timu hiyo Juma Mwambusi ameweka wazi.
“Hapa Comoro ni karibu unajua sheria ya mashindano inataka masaa 72 kabla ya mchezo au unaweza ukawahi sana kwa ajili ya hali ya hewa au ukachelewa kidogo kama hali ya hewa ya mahali ulipotekea haitaleta matatizo, halafu ni mwendo wa saa moja na nusu sasa muda huo hauwezi kuathiri chochote”
Ili usipitwe na Breaking NEWS zote za Tanzania na nje ya Tanzania, matukio ya habari za mastaa, michezo na mengine, usiache kujiunga na Millard Ayo kwa ku-subscribe Youtube jina la “millardayo” pia Install APP ya “millardayo” kwenye Android na IOS, Facebook, Twitter na Instagram @millardayo