Baada ya ubishi uliyoanzia October 1 2016 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Simba kumalizika kwa sare ya 1-1, huku mashabiki wa Simba wakilalamika kuonewa na kuvunja viti, February 25 2017 katika mchezo wa marudiano majibu yamepatikana.
Simba na Yanga wamerudiana katika mchezo wa round ya pili uwanja wa Taifa Dar es Salaam, katika mchezo huo wa marudiano Simba wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, magoli ya Simba yakifungwa na Laudit Mavugo dakika ya 66 na Shiza Kichuya aliyefunga akitokea benchi.
Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 4 kupitia kwa Simon Msuva kwa mkwaju wa penati, hiyo ni baada ya Obrey Chirwa kuchezewa faulo katika eneo la hatari, ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuongoza Ligi kwa jumla ya point 54 katika msimamo wa Ligi Kuu Vodacom.
Yanga sasa wanabaki kuwa na point zao 49 wakiwa wamecheza mchezo wao wa 22 leo lakini wana mchezo mmoja wa kiporo, Simba ambao wanaongoza Ligi kwa sasa wamecheza jumla ya michezo 23 ya Ligi Kuu Vodacom na wamesalia na mechi saba tu kabla ya Ligi kuisha.
FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5