Rekodi ya Dunia ya watu wanaoaminika kuwa na akili nyingi zaidi (IQ) ni Wanasayansi na wachezaji Chess lakini pia unaweza ukawa umewahi kujiuliza ni kiongozi gani mwenye akili zaidi Duniani, nimekutana na list hii kutoka www.topteny.com inakuletea majina ya viongozi waliothibitika kisayansi kuwa na IQ kubwa zaidi duniani.
1:Benjamin Netanyahu (Israel) – IQ=180
Huyu ni Waziri mkuu wa Israel na anatajwa kuongoza kuwa na IQ ya 180, kwa mujibu wa score za IQ, Benjamin Netanyahu anauwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo na kutatua maswali magumu.
2: John Quincy Adams (USA) – IQ=175
Alikuwa Rais wa sita wa Marekani kuanzia mwaka 1825 mpaka 1829 ana IQ level ya 175 , ambayo ni kubwa zaidi ukilinganisha na marais wengine wa Marekani.
3: Joachim Palme (Sweden) – IQ=156
Waziri mkuu wa sita wa Sweden Joachim (1969-1976), ukiacha mchango wake mkubwa katika kuchangia nchi nyingi kupata uhuru pia anaweka rekodi ya kuwa kiongozi namba tatu kuwa na IQ kubwa zaidi Duniani.
5: George Washington (USA) – IQ=140.
Rais wa kwanza wa Marekani George Washington anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa wa kuiletea uhuru Marekani pia anatajwa kuwa katika list ya viongozi 10 wenye IQ ya 140.
6: Thomas Jefferson (USA) – IQ=138
Thomas Jefferson anatajwa kama Rais aliyechangia maendeleo ya mwanzo ya Marekani, wanasayansi wanamtaja kuwa na IQ level ya 138.
7: Richard Nixon (USA) IQ =132.
Baada ya kujiuzulu kwenye kiti cha urais Richard Nixon alipata upinzani mkubwa sana lakini hiyo haikumuondolea sifa ya kuwa kwenye list ya viongozi wenye IQ kubwa, ambapo ana IQ ya 132.
8: John F. Kennedy (USA) – IQ=117.
Alikuwa Rais wa 35 wa Marekani na Rais mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa na taifa hilo akiwa na umri wa miaka 43 tu wakati huo, Kennedy anatajwa kuwa na IQ level ya 117.
9: Ferdinand Marcos (Philippines) – IQ=98.01
Anajulikana kama Rais aliyeshikilia kiti cha Urais kwa muda wa miaka 20, anatajwa kuwa na IQ ya 98.01
10: Dr. Ing. Bacharuddin Jusuf Habibie (Indonesia) IQ = 97.0 1
Akiwa na umri wa miaka 38 tu alitajwa kama mtu mwenye IQ kubwa baada ya kugundua teknolojia ya kupunguza ajali za ndege, alitajwa kuwa na IQ level ya 97.1
AyoTV MAGAZETI: Makonda amwaga machozi kanisani, Gwajima azindua ‘oparesheni’ mpya