Kwa mujibu wa utafiti uliofanya na umoja wa mataifa ‘UN’ umedai kuwa takribani watu laki mbili hufa kila mwaka kutokana na sumu inayotokana na madawa yanayopulizwa kwenye mazao ya chakula.
Ripoti hiyo imesema dawa zinazopulizwa kwenye mazao zinasaidia kuzuia wadudu wanaoshambulia mazao lakini pia zina madhara makubwa sana kwa afya ya binadamu na husababisha magonjwa hatari kama cancer, Alzheimer’s na Parkinson’
Akizungumza na Aljazeera msemaji wa masuala ya mazingira kutoka umoja wa mataifa alisema nchi zinazoendelea hasa kutoka Afrika ziko katika hatari ya vifo vinazosababishwa na watu kutumia dawa zenye kemikali yenye sumu kumwagilia mazao yao.
VIDEO: Waliozaliwa baada ya 1990 wana hatari ya kupata kansa ya utumbo, Bonyeza play hapa chini kutazama