Leo March 20, 2017 kupitia Clouds TV/ FM na Choice FM, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amezungumza kuhusu taarifa zilizosambaa mitandaoni Wikiendi iliyopita juu ya kuvamiwa kwa kituo hicho wakati shughuli za vipindi zikiendelea.
Nimekukusanyia kila kitu alichokizungumza Ruge Mutahaba leo.
'Interview ya leo ilipangwa, leo tulikuwa tuzungumzie ishu ya Malkia wa Nguvu, ingawa kuna mengine yametokea hapa katikati' -Ruge #Clouds360 pic.twitter.com/kPdFxSoSMG
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
'Alhamisi asubuhi tulikuwa na kikao na Kamati ya Maudhui TCRA walikuja kutupatia msasa kidogo, akaja Mkuu wa Mkoa Makonda' -Ruge #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Katikati ya kikao Makonda alitutembelea tukaongea mambo kadhaa tukaagana na watu wa TCRA' – Ruge #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Wakati natoka ofisini nilikutana na Makonda na Vijana wa SHILAWADU nikauliza kwema hapa nikajibiwa ni Story za kawaida tu' Ruge #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Nikiwa kwenye gari alinifata mmoja wa watangazaji wa kipindi cha SHILAWADU kuniambia kuhusu mwanamke aliyezaa na Gwajima -Ruge #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Nikawauliza hiyo story mna uhakika nayo mmeibalance mmempata Mchungaji Gwajima? nilimpigia Mkuu wa Vipindi Kerry kumuuliza'-Ruge #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Nilitoa maelezo kwa boss wa vipindi CloudsTV kuhusu kipindi kisichokuwa na maana sababu hakija balance na kisiruke hewani' -Ruge #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Saa 10 Alhamisi nilipata Simu ya Gwajima kunieleza kuhusu kuwepo kipindi kinachomuhusu nikamueleza hiyo story haitoruka-RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
'Nilimueleza Kerry ambaye ni kiongozi awasiliane na Makonda kwamba video yake haitoruka hewani sababu haija balance' -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Ijumaa Saa 5 kasoro nilipokea simu kutoka kwa HR wetu kwamba RC Makonda ameingia ofisini akiwa na askari sita wenye silaha -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Baadaye nilipata simu toka kwa Mkurugenzi Mtendaji Joseph Kusaga kwamba anapewa lawama na RC Makonda tumezuia kipindi chake'-RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Nikaamua kumpigia simu Mkuu wa Mkoa Makonda nikamuuliza ni nini hicho umefanya kwanini hakunipigia mimi kwanza' -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Nilipata maelezo kutoka kwa Sam aliyekuwepo mapokezi akanieleza RC Makonda alikuwa anachukua kitu kwenye flash' -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Kwa Mara ya kwanza Makonda anatuvunjia heshima sisi kama rafiki zake tulifanya kazi naye vizuri tangu akiwa Mkuu wa Wilaya -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Ukweli sisi kama chombo cha Habari lazima tujenge heshima ya kutoa habari zenye uwiano lazima tuiheshimu tasnia yetu- RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Hofu yangu ni kwamba kama mimi nipo na mkurugenzi yupo kwanini asingetengeneza mazingira ya kuonana na sisi kwanza-RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Naomba nieleweke wazi hatuwezi kumuacha mtu akatupanda kichwani hii ni dharau kwangu nasimamia watu zaidi ya 200 asinidharau-RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Panapotokea misingi ya hofu lazima tuweke wazi kabisa bila kificho panopohitaji ukweli lazima tuweke wazi ukweli usemwe-RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Mfano wangu ni kwa timu za Simba na Yanga ni mahasimu lakini chombo kinachowasimamia kikiingilia maslahi yao wanaungana -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Nimefurahi wanaoitwa mahasimu wetu wa Majizo alitupigia simu, Mengi atafika leo kututembelea Tasnia yetu lazima ilindwe -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Mimi sitaki kuona bunduki mtaani kwa maslahi ya vizazi vya kesho, bunduki ziwepo wanapolinda benki sio kwenye media- RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Tuhukumiwe kama taasisi napenda vijana wapende kutengeneza kesho yao kwa Uhuru lakini sio kwa chuki za kupandikizwa na watu -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Vijana wa SHILAWADU wapo kwenye hofu wametishwa wamepoteza morali na kazi yao hawana Amani tena wameomba likizo -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Kwenye uchaguzi wanasema mtu akikufuata kukupa rushwa chukua lakini kura ni maamuzi yako mwenyewe -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Unakwendaje kutoa kitu kwa mtu asiye na maamuzi na jambo huo utakuwa ni ujinga wako mwenyewe -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Sisi tunampenda Makonda hatulipi chochote tunaipenda Dar es Salaam tulifanya kampeni ya 'Dar Mpya' kwa mapenzi yetu wenyewe -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Sakata hili lisihusishwe na kutetea vita dhidi ya madawa ya kulevya kama mtu kakosea ni kakosea tu kwa utashi wake -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Sisi tuna namna yetu ya kuadhibiwa tunahitaji kuwe na Uhuru wa habari, sio kwakua una mamlaka fulani ukatupanda kichwani -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Viongozi wetu wanapenda kumtaja Mungu lakini matendo yao ni tofauti watu wanaumia kwenye hili -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Tukiongea kwa watu wanasema tunahitaji mtu atumbuliwe lakini sisi tunaongea kwa nafasi yetu tumeumia kwenye hili -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Sisi Clouds Media bahati mbaya tumekuwa ni watu wa kuzungumza na watu tunapokosea watu wanatuwajibisha moja kwa moja -RUGE #Clouds360 pic.twitter.com/ky82sWcvNG
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Nikwambie siri moja Ruge kama ungesema tofauti mimi ningepata tabu sana kufanya kazi CMG kwa nilichokiona mtandaoni-MasoudKipanya #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Suala ni kwamba tulifikiri ni mapungufu ya kibinadamu ina maana Makonda hakujua kuna Camera kila mahali, jambo la kutafakari-RUGE #Clouds360 pic.twitter.com/r7uSvvjYZ7
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Hapo kweli ni Clouds, Jumamosi tulidhani anaweza kuomba radhi, na kwenye mitambo ya CCTV kila mtu anapafahamu -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Makonda ni mdogo wangu sana anaweza kuniomba msamaha, akumbuke mimi nawakilisha kundi la watu waliokosewa kwenye hili -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Kitu kibaya ambacho kinaumiza moyo RC Makonda ametumia vibaya madaraka yake pamoja na urafiki wake kwetu kama Media -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Hatua ya maamuzi yetu bado tupo kwenye mashauriano hatutaki kupingana na ajenda za serikali kwa sasa, tutaamua cha kufanya -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Tulikuwa tunaonekana hiki ni kitu cha Makonda lakini viongozi wengi hawatumii fursa wenye ajenda ya maendeleo waje hapa -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Sisi sio viongozi ni wananchi tuna miaka 20 kama chombo cha Habari tunakaribisha agenda zenye ubunifu, tujadiliane pamoja -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Sisi kama Clouds Media tumeumia kuona tukio hili limetokea tena kwa mtu wetu ambaye angeweza kuhoji kwa njia nzuri -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Toka jambo hili litokee binafsi bado sijafanya mazungumzo yoyote na Mkuu wa Mkoa' – RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Ni kweli pale Clouds na sijui kaachia nani zile video, Ni kweli tuna Cctv kila sehemu maana hili ni jengo la habari – RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
Tusimpe kazi ngumu Rais, huyu baba anatakiwa kuangalia maendeleo yetu, nimesema leo niongelee hili tuendelee na kazi -RUGE #Clouds360
— millardayo (@millardayo) March 20, 2017
VIDEO: Magazeti ya leo March 20, 2017 tayari nimekuwekea hapa, Bonyeza play kutazama