Siku moja baada ya kuapishwa kwa waziri mpya wa wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe alijitokeza uwanja wa Taifa Dar es Salaam kutazama mchezo wake wa kwanza wa Taifa Stars dhidi ya Botswana kwa mara ya kwanza toka ateuliwe kuwa waziri wa michezo.
Waziri Mwakyembe alikuwepo uwanja wa Taifa kutazama mchezo huo uliyomalizika kwa Tanzania kupata ushindi wa goli 2-0 lakini alikutana na kusalimiana na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo mbunge wa Mtana Nape Nnauye na kufurahia kwa pamoja ushindi wa Taifa Stars.
ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1