Baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, kuliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Nay wa Mitego ambaye alikuwa akishikiliwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za wimbo wake wa ‘WAPO’ kutokuwa na maadili, Nay wa Mitego ametoka kituoni hapo leo March 27 2017.
Nje ya kituo hicho cha Polisi Nay wa Mitego amezungumza na waandishi wa habari na kusema………>>>’Asante kwa wote walioamka na kuwa upande wangu, upande wa haki, walioamini kile ambacho nimekifanya nawashukuru sana‘-Nay wa Mitego
Unaweza kubonyeza play hapa chini kuitazama
VIDEO: Sababu za Waziri Mwakyembe kuagiza Nay wa mitego kuachiwa, Bonyeza play kusikiliza