April 2 2017, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya uchaguzi wa Wabunge watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Afrika Mashariki ambao walihitajika Wabunge Tisa.
Baada ya uchaguzi huo, ni wabunge saba; wabunge sita kutoka CCM na mmoja CUF wamepatikana huku wabunge wawili wa CHADEMA wakipigiwa kura ya hapana hivyo kufanya kuwa na pengo la Wabunge wawili ili kukamilisha idadi inayotakiwa kwa mujibu wa Mkataba wa Afrika Mashariki unaozitaka kila nchi mwanachama Wabunge Tisa.
Leo April 8, 2017 Ayo TV na millardayo.com ilimtafuta Wakili wa kujitegemea Jebra Kambole ambaye pia ni Mwanasheria wa Haki za Binadamu Tanzania ili kufafanua kitu gani kitaendelea baada ya tukio hilo na iwapo Wabunge hao saba wataapisha ili kuendelea na shughuli za EALA.
“Kanuni zinaelekeza kwamba, upige kura za tiki kwa watu tisa, halafu ukaweka tiki kwingine ukaweka kosa. Je, hiyo kura itakuwa halali au siyo halali? Ni miongoni mwa changamoto za kisheria ambazo zimejitokeza katika uchaguzi huu…” – Jebra Kambole.
Hapa Wakili Kambole anafafanua…
VIDEO: Matokeo ya wabunge wa A. Mashariki yalivyotangazwa Bungeni Dodoma. Bonyeza play kutazama.