Staa wa soka wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Neymar amekutana na adhabu ya kufungiwa mechi 3 kuichezea FC Barcelona na shirikisho la soka Hispania ( Royal Spanish Football Federation (RFEF) kwa makosa mawili.
Neymar amefungiwa mechi tatu, mechi moja ni kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano wakati wa mchezo dhidi ya Malaga uliyomalizika kwa FC Barcelona kupoteza kwa magoli mawili kwa 2-0 lakini mechi ya mbili kwa kosa la kumpongeza kwa kejeli fourth official wakati anatoka nje ya uwanja.
Mchezaji huyo raia wa Brazil alitoa lugha za kejeli kwa fourth official wakati anatoka uwanjani kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano, refa wa game hiyo Jesus Gil Manzano ndio aliandika ripoti hiyo, Neymar sasa atakosa mchezo dhidi ya Real Sociedad, Real Madrid na Osasuna.
VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera April 2 2017