Staa wa soka wa kimataifa wa Ivory Coast aliyewahi kuichezea Chelsea ya England kwa mafanikio Didier Drogba amerudi kwenye headlines za soka kwa mara ya kwanza toka aachane na timu ya Montreal Impact.
Drogba mwenye umri wa miaka 39 aliachana na Montreal Impact kwa miezi kadhaa na kukaa bila timu licha ya kuwa alipokea ofa nyingi kutoka katika timu za England, China, Ufaransa na timu ya Corinthians ya Brazil baada ya kuichezea Montreal kwa miezi 18.
Leo Drogba ametangazwa kujiunga na timu ya Phoenix Rising FC ya Marekani iliyopo daraja la tatu (American’s United Soccer League) kama mchezaji na sehemu ya mmiliki wa timu hiyo ambayo sio maarufu.
Drogba ana malengo ya kuiwezesha Phoenix ishiriki Ligi Kuu Marekani (MLS) mkataba wa kuichezea timu hiyo unaweza kuwa wa misimu miwili au mitatu kabla ya kuamua kuwa kocha au sehemu ya utawala wa timu hiyo, Drogba ana hisa katika timu hiyo.
VIDEO: Simba ilivyobadilisha matokeo vs Mbao FC dakika za mwisho Mwanza