Siku kadhaa zimepita toka club ya Dar es Salaam Young Africans ikataliwe na shirikisho la soka Tanzania TFF kuutumia uwanja wa CCM Kirumba katika mechi dhidi ya MC Alger iliyochezwa April 8 uwanja wa Taifa kwa kigezo kuwa uwanja huo hauna vigezo.
Kwa kawaida mechi za kimataifa zinaruhusiwa kuchezwa katika viwanja vyenye viwango na vilivyoidhinishwa na FIFA na CAF lakini CCM Kirumba haikuwa imepitishwa hivyo Yanga kushindwa game vs MC Alger katika uwanja CCM Kirumba.
Good news ikufikie aliyoitangaza leo Rais wa TFF Jamal Malinzi kupitia ukurasa wake wa twitter ni kuwa CAF na FIFA wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba utumike katika mechi za kimataifa, hivyo timu za Tanzania zitakuwa na uhuru wa kutumia uwanja wa Taifa au Kirumba.
EXCLUSIVE: Mishahara ya kwanza ya mastaa wa soka Samatta, Msuva, Maguli, Himid Mao na Bossou