Utafiti uliofanywa na European Bank for Reconstruction and Development ‘EBRD’ umebaini kuwa, kwa kila 10% inayoongezeka kwenye bei ya nyumba, kiwango cha jumla cha uzazi hupungua kwa 1.3%.
Katika stori iliyochapishwa na Daily Mail April 13, 2017, inakadiriwa kuwa watoto wapatao 700,000 huzaliwa kila mwaka katika nchi za Uingereza, lakini ongezeko la bei ya nyumba katika uwiano huo kunaweza kupunguza idadi hiyo kwa zaidi ya watoto 7,000.
Hali hiyo ni tofauti kwa wanaomiliki nyumba zao ambapo kwa ongezeko la 10% kwenye bei ya kodi ya nyumba, husababisha ongezeko la vizazi kwa 2.8%. Miongoni mwa wapangaji, hata hivyo, ongezeko hilo husababisha kushuka kwa kiwango cha uzazi kwa 4.9%.
Dr Cevat Giray Aksoy, ambaye alifanya utafiti nchini England, alisema wapangaji hulazimika kusitisha kupata watoto mpaka watakapokuwa mahali sahihi.
“Utafiti huu unasapoti dhana kwamba gharama za nyumba hushusha presha kwenye matokeo ya ustawishaji kwa watu wa rika la kati na hii kuna uhusiano baina ya kuwa sehemu sahihi na kujenga familia.” – Dr Cevat Giray Aksoy.
Wataalamu wanaonya kuwa baadhi ya couple ambao husitisha kupata watoto mpaka watakapokuwa vizuri kiuchumi wako hatarini zaidi watakapojua kuwa wamechelewa.
AyoTV MAGAZETI: Ulikosa kilichoandikwa kwenye magazeti ya April 14, 2017? Bonyeza play kutazama.