Mtanzania Mbwana Samatta ambaye kwa sasa Tanzania ina mtazama kama balozi wa soka la Tanzania barani Ulaya akiwa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji, ameonekana kuwa na tabia ya kupenda kushea vitu vya kitanzania na wachezaji wenzake wa KRC Genk.
Samatta aliwahi kupost video kupitia ukurasa wake wa instagram akiwaonesha wachezaji wenzake Omar Colley kutoka Gambia, Leon Bailey raia wa Jamaica ambaye kwa sasa anaichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani wakicheza wimbo wa ‘Muziki’ wa Darassa.
Leo kupitia ukurasa wake wa instagram ikiwa siku moja imepita toka wacheze game yao ya robo fainali ya Europa League dhidi ya Celta Vigo na kupoteza kwa magoli 3-2, amempost mchezaji mwenzake raia wa Uholanzi Jean Boetius akisoma lugha ya Kiswahili.
Inawezekana Samatta anajaribu kumfundisha maneno machache ya lugha ya kiwaswahili Jean Boetius, kama utakumbuka Boetius ndio mchezaji wa KRC Genk aliyeifungia KRC Genk goli la kwanza dakika ya 10 jana dhidi ya Celta Vigo.
Inawezekana @samatta77 kaanza kumfundisha mchezaji mwenzake wa KRC Genk Jean Boetius raia wa Uholanzi lugha ya kiswahili #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/D0aaA8C5bQ
— millard ayo (@millardayo) April 14, 2017
VIDEO: Simba ilivyobadilisha matokeo vs Mbao FC dakika za mwisho Mwanza