Siku moja baada ya Kamati ya saa 72 kupitia Mwenyekiti wake Hamadi Yahaya kutangaza kuwa Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilimchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, Kagera Sugar wameandika barua ya kuomba shauri lao lisikilizwe tena.
Kagera Sugar imefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa mchezaji wao Mohamed Fakhi hana kadi tatu za njano kama ambavyo wameadhibiwa na kupokonywa point na bodi ya Ligi, hivyo wanaomba lipitiwe upya shauri lao na kuhakikisha haki inatendeka.
Kama utakuwa unakumbuka Simba na Kagera Sugar zilicheza game April 2 2017 katika uwanja wa Kaitaba Bukoba na Simba ikapoteza kwa kufungwa magoli 2-1, ila baada ya hapo walikata rufaa kwa kuituhumu Kagera Sugar kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu kinyume na taratibu.
Baada ya kupokonywa point na kupewa Simba, Kagera Sugar wameomba lipitiwe upya shauri lao kuhusu Mohamed Fakhi kuwa na kadi 3 za njao. pic.twitter.com/FkLkdMCelo
— millard ayo (@millardayo) April 14, 2017
VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera Sugar leo April 2 2017