Baada ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wa kwanza wa kuwania kuingia hatua ya Makundu Kombe la shirikisho April 8 uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0, leo April 15 ilikuwa ni zamu ya kucheza Algeria mchezo wa marudiano.
April 15 nchini Algeria katika uwanja wa July 5 1962 mjini Al-Jaza’ir, Yanga ambao waliingia wakiwa wanahitaji sare ya aina yoyote ili waweze kupata nafasi ya kuingia katika hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho barani Afrika, wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 4-0 na safari yao kuishia hapo.
Magoli ya MC Alger ambao waliingia uwanja wa July 5 1962 wakiwa na sapoti kubwa ya mashabiki wao yalifungwa na Aouadj dakika ya 14 na 91, Derrardja dakika ya 39 na Zerdab dakika ya 66, hivyo Yanga wanaondolewa katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika kwa jumla ya magoli 4-1.
VIDEO: Game haikuoneshwa Yanga vs MC Alger, nimeyanasa matukio na goli la Yanga FT 1-0