Siku chache baada ya mastaa wa Bongo movie kuandamana hadi Kariakoo wakitaka filamu za kigeni zizuiliwe nchini, kumeibuka hoja mbalimbali huku watu wengi wakioneshwa kutofurahia uamuzi huo.
Miongoni mwa watu waliotoa maoni yao kwa kuguswa stori ya Bongo movie ni staa rapa kutoka Weusi ambaye pia ni msemaji wa kundi hilo Nikki wa Pili ambapo kupitia account yake ya Twitter amewaandikia ujumbe wasanii wa Bongo movie akisema asanii hao wanafahamika kwa mambo mengine zaidi kuliko hata movie zao akiwapa ushauri wa kulinda kazi zao kama wafanyavyo wasanii wa nje.
>>>“Movies za rambo ni maarufu kuliko rambo mwenyewe, bongo movies tunawajuwa kwa vitu vingine zaidi wala hata sio movie zao. Ni kweli tunahitaji kulinda soko la ndani, la movies lakini wao wanahitaji kufanya tafakuri ya kina.
“Bongo movies mwanzoni walikuwa na soko, kuanza ni kujaribu, but ku sustain is a science… mwendelezo wa lolote huitaji maarifa. Nchi zote zilizoendelea zililinda masoko ya nyumbani, ndio tulilinde lakini wenye movie nao wajilinde kwa kujiongeza kila kukicha.” – Nikki wa Pili.
VIDEO:Yusuph Mlela ameomba pambano la ngumi na Nay wa Mitego…