Tunafahamu kwamba serikali imepiga marufuku utumiaji na biashara ya vinywaji aina ya viroba, Mbunge wa Gairo Ahmed Shabiby alisimama bungeni na kuishauri serikali namna bora ambayo ingetakiwa kutumia kuzuia usambazaji wa vinywaji hivyo ikiwa ni pamoja na kuzuia bidhaa kutozalishwa viwandani kwanza na sio kuwakamata wauzaji kama inavyofanya hivi sasa.
Shabiby amesema>>> ‘Katika bajeti ya mwaka jana wakati tunaweka kodi katika vinywaji hata viroba navyo tulivihesabu na vilikuwepo kihalali, ni kweli pombe hii inadhuru watu lakini nashauri wakati mwingine utaratibu utakaotumika kuzuia uanzie kwenye viwanda’
Full video nimekuwekea hapa chini tayari….
VIDEO: ‘Kwani serikali mna matatizo gani?’ –Mbunge Susan
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo