Staa wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Chelsea ya England N’golo Kante amefanikiwa kushinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka wa England kwa kuwashinda Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez kwa kupata kura nyingi.
Dele Alli wa Tottenham ameshinda tuzo ya mchezaji bora mdogo wa PFA wakati Lucy Bronze wa Man City ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike, huku mkongwe wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England David Beckham akishinda tuzo ya heshima kwa mchango wake katika soka.
N’golo Kante alikuwa mchezaji muhimu na kuisadia Leicester City kutwa Ubingwa wa EPL msimu uliyopita na sasa yupo Chelsea iliyopo katika mbio za Ubingwa ikiwania na Tottenham Hotspurs, kama atafanikiwa kutwaa taji la EPL atakuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufanya hivyo mara mbili mfululizo akiwa na timu mbili tofauti.
Kante ameichezea Chelsea takribani kwa dakika zote msimu huu katika EPL kasoro mechi iliyochezwa siku ya Boxing Day dhidi ya Bournemouth ambapo alikuwa kafungiwa na dakika 11 za mwisho za mchezo dhidi ya Tittenham Hotspurs January 4 2017.
VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba na kamati ya nidhamu ya TFF