Baada ya hivi karibuni kuripotiwa taarifa kuwa kuna utafiti uliofanywa kwenye mafuta ya Alizeti ambayo huelezwa kuwa salama zaidi kwa watumiaji huku utafiti huo ukionesha kuwa mafuta hayo ni hatari kutokana na kusababisha tatizo la Kansa kwa watumiaji.
Leo April 24, 2017 Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA imetoa ufafanuzi juu ya utafiti huo na kueleza kuwa mafuta hayo ni salama kwa watumiaji lakini iwe ni yale yaliyothibitishwa na Mamlaka hiyo, pia imeeleza kuwa utafiti huo ulifanywa kwenye mbegu na mashudu pekee ambayo yalionesha kuchafuliwa na sumu ya Aflatoxin.
Hivyo basi TFDA imefanya uchambuzii wa wa awali wa matokeo ya utafiti huo na itafanyia uchunguzi ripoti ya utafiti huo uliochapishwa na jarida la PLOS One kwenye mafuta na mbegu zinazozalishwa hapa nchini ili kubaini kama kuna tatizo hilo.
Taarifa kamili nimekuwekea hapa chini
VIDEO: Ilikupita hii ya maswali ya Mbunge Goodluc Mlinga na Majibu ya Naibu Waziri Kigwangalla? Itazame hapa chini