Jukwaa la Wahariri Tanzania ‘TEF’ leo April 26, 2017 limekutana na waandishi wa habari kuzungumzia tukio la kushambuliwa kwa waandishi wa habari wakati wanatekeleza wajibu wao kitaaluma Jumamosi April 22, 2017.
Katika tukio hilo waandishi wa habari walishambuliwa na wafuasi wa CUF upande wa Prof. Ibrahim Lipumba ambapo kutokana na kitendo hiko, TEF wametoa msimamo wao ikiwa ni pamoja na kumtaka Prof. Lipumba kutoa kauli binafsi kama alivyofanya Maalim Seif aliyeandika barua kwa TEF akilaani kupigwa kwa wanahabari hao na kutoa pole.
Akieleza kusikitishwa kwake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Theophil Makunga amesema: “Jukwaa la Wahariri Tanzania limeshtushwa kushambuliwa na kuumizwa kwa waandishi wa habari ambao walikuwa wakitekeleza wajibu wao kitaaluma mwishoni mwa wiki iliyopita.” – Theophil Makunga.
Bonyeza play kutazama…
VIDEO: “Hatuna sababu ya kukataa, sisi tulituma vijana wetu”- CUF. Bonyeza play kutazama…