Kufuatia tetemeko llililotokea kwa mara nyingine mkoani kagera majira ya saa 7 na dakika 29 za usiku wa kuamkia April 30 mwaka huu,mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu amesema kuwa tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa 3.1 vipimo vya ritchel.
‘Wanasema lile tetemeko lilitokea ziwani eneo la Minziro, zile ni after shocks za lile lililotokea mwaka jana mwezi wa tisa na wanasema ni vizuri yaendelee kutokea hayo madogomadogo kuipa nafasi miamba ipumue kuliko kukaa muda mrefu miaka na miaka alafu linatokea kama lile la mwaka jana’–RC Kijuu
‘Wanasema hizi after shocks zitakuwepo na zitaendelea kuwepo ni miamba inapumua,muhimu tuzingatie yale tuliyokuwa tunashauliwa na wataalamu mbalimbali wa miamba waliokuja na tuachane na taaruki‘-RC Kijuu
Full video nimekuwekea hapa chini tayari…
EXCLUSIVE: Mashuhuda wasimulia tetemeko lilivyotokea Kagera usiku
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo