CITIZEN TV ya Kenya imeripoti taarifa ya wizi wa punda uliokithiri huko Turkana kiasi kwamba hata Wakazi wenyewe wamejawa na hofu na kisa kikiwa ni kuuzwa kwa ngozi ya punda hao.
Biashara ya kuuzwa ngozi ya punda inadaiwa kuwa imeletwa na Wachina na kufanya ngozi ya mnyama huyo kupanda thamani hadi shilingi za Kenya 10,000 ambazo ni zaidi ya shilingi laki mbili za Tanzania huku Punda mwenyewe akiuzwa Ksh 5000 (laki moja na elfu nane ya Tanzania).
Wanasema baada ya Wachina kuinunua ngozi hiyo husafirishwa na kwenda kutumika kwenye kutengeneza dawa inayotibu magonjwa mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.
...>>>”Unaweza nunua punda kwa elfu 5 au sita na ukauza ngozi kwa Elfu 10 hali hiyo ikaleta thamani ya Punda na ndiomaana wezi wanaiba Punda na kumchuna ngozi ili aje auze ngozi peke yake” – Joseph Losuru
“Tuliona kwenye media za Nigeria kuwa Punda wameisha lakina na hapa kwetu pia Punda wameanza kuisha” – Lokwale Anton Mfugaji
Tazama Taarifa ya Habari ya Azam Two May 6 2017
https://youtu.be/76vTVhWWVss
VIDEO: Ni Tundu Lissu na Joseph Mbilinyi tena bungeni, KILA KITU KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI