Wizara ya Afya imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola hasa katika mikoa ambayo inapakana na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuripotiwa wagonjwa wa ugonjwa huo nchini humo.
Hatua hii inakuja baada ya Shirika la Afya Duniani ‘WHO’ May 12, 2017, kutangaza kulipuka kwa ugonjwa wa Ebola katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika Jimbo la mpakani na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wizara ya Afya imeomba kutengewa Trilion 1.1 kama bajeti yake…