Misaada kutoka MULTICHOICE Tanzania ilikuwepo siku nyingi na kinachofanywa sasa ni muendelezo tu wa kilichoanzishwa ambapo mara nyingi tumeshuhudia jinsi wanavyogusa wasiojiweza huku mitaani kwa misaada mbalimbali.
Leo ni zamu ya Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale, DSM kwa kuwapa zawadi za vyakula mbalimbali kwa ajili ya Eid ikiwa ni miaka mitano sasa kwa Multchoice kutoa misaada mbalimbali kwenye kituo hicho wakitambua malezi ya watoto waishio kwenye mazingira magumu ni jukumu la kila mtu.
Meneja Operesheni wa Multichoice Baraka Shelukindo ndiye alisimamia hili zoezi mwanzo mwisho akishuhudiwa na baadhi ya mabalozi wa DStv akiwemo Hadija Kopa na Riyama Ali ambapo mbali na kukifadhi kituo hicho mara kwa mara pia walifadhili uanzishwaji wa mradi wa ushonaji.
>>> “Tunatambua kuwa jukumu la kuwalea watoto kama hawa ambao kwa sababu moja ama nyingine wamejikuta katika mazingira magumu ni letu sote. Hawa ni ndugu zetu, watoto wetu, na pia ni tegemeo kubwa kwa taifa letu, hivyo kuwasaidia ni jukumu letu.” –Shelukindo.
Al-Madinnah Orphanage Centre ni kituo kilichoanzishwa mwaka 2004 ambapo hadi sasa kinahudumia watoto 65 ikiwa ni wavulana 40 na wasichana 25 huku wengi wao wakiwa wanafunzi wa Shule za Msingi.