Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM katika kuhakikisha linadumisha amani na usalama msimu huu wa Sikukuu limesema litatumia vikosi vyake vyote kusimamia amani na usalama maeneo mbalimbali zikiwemo kumbi na sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM Lucas Mkondya amesema Jeshi hilo limejipanga kuhakikisha Watanzania wanasherehekea vizuri Sikukuu:>>>”Napenda kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM tumejipanga vyema sana. Kwa hiyo Wananchi wajiandae tu kwa sherehe, Jeshi liko vizuri.
“Tutakuwa na Ulinzi wa kutosha, Askari watakuwepo wote hakuna Askari ambaye atakuwa na Sikukuu. Tumeitisha Askari wote na tumepata Askari kutoka vikosi vingine nje ya Kanda Maalum ambao watakuja kushirikiana nasi. Katika kuwahakikishia kwamba kila ambapo patakuwa na mkusanyiko wa watu, Askari watakuwepo wa kutosha.
“Nyumba zote za Ibada tutaweka Askari. Kutakuwa na Askari wa kawaida wenye Uniform lakini pia kutakuwepo na Askari kanzu kufuatilia nani anataka kufanya vurugu katika nyumba za Ibada lakini pia katika sehemu ambazo Wananchi wataenda kufanya Sherehe.
“Tutatumia katika kuhakikisha ulinzi unaimarika tutatumia Vikosi vyetu vyote. Tutatumia Vikosi vya FFU vitakuwepo mitaani kwa ajili ya kuimarisha Doria. Tutatumia Helkopta, tutatumia Farasi, tutatumia Mbwa na Askari wengi sana watakuwepo. Kwa hiyo napenda kuwahakikishia Wananchi kwamba wasiwe na wasiwasi Jeshi lao la Polisi limejipanga katika kuwalinda na kuhakikisha kwamba Sikukuu Eid Mosi, Eid Pili zinapita salama bila kubughudhiwa.” – Lucas Mkondya.
Polisi DSM wazungumzia tukio la Walemavu kupigwa mabomu!!!