Moja ya story kubwa iliyosomwa katika Taarifa ya Habari ya Saa Moja Usiku kupitia Channel Ten ni hii kuhusu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo DSM John Kayombo kuamuru Wahasibu wa Manispaa hiyo kuwekwa mahabusu.
Mbali na Wahasibu hao pia vibarua wawili kutoka katika kituo cha mabasi cha simu 2000 wamewekwa mahabusu baada ya kubainika kufanya ubadhilifu wa pesa kwa kutoa huduma ya Vyoo bila kutoa risiti ya mashine huku wakiwasilisha kiasi kidogo cha pesa tofauti na makusanyo ya siku.
“Wahasibu wangu ambao nimewaamini nimewaweka hapa hawatoi risiti zote. Risiti za kuoga hazitoki na wala wanaolipwa hizi fedha ambao ni wakusanyaji pia hawatoi risisti.
“Wizi ni mkubwa lakini nataka wanielewe kipindi hiki ni cha kazi. Tunataka watu wafanye kazi. Muhasibu wa mapato nimemwambia ajitathimini kama anatosha kuendelea kuwa Muhasibu wa mapato wa Halmashauri. Kesho aniandikie barau kama anataka kuendelea au hataki kuendelea astep down tumpe kazi mtu mwingine.” – John Kyombo.
“Tutatumia vikosi vyetu vyote; Helkopta, Farasi na Mbwa” – Polisi DSM
UFAFANUZI: Wauza Unga kuishi kifahari gerezani, Sianga kutishiwa kifo