Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi anaweza akakutana na adhabu ya kifungo cha miezi 21 jela yeye pamoja na baba yake mzazi Jorge Messi kwa kosa la ukwepaji kodi Hispania katika kipindi kati ya mwaka 2007 hadi 2009.
Lionel Messi na baba yake wanatajwa watahukumiwa kifungo kwa kosa la kukwepa kodi, Messi sio staa wa kwanza wa FC Barcelona kuingia katika kashfa ya ukwepaji kodi, aliwahi kuhukumiwa beki wa timu hiyo Javier Mascherano mwaka mmoja jela January 21 2016 lakini alinusurika kwenda jela kwa kulipa faini.
Hivyo kwa kosa la Lionel Messi kudaiwa kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 jela anaweza kukikwepa kwa kulipa faini ya dola 285,000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 637.8, Sheria ya Hispania mtu akihukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili ana nafasi ya kuomba adhabu yake ibadilike kutoka kifungo kuwa faini, kama tu kosa lake likiwa sio la jinai.
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1