Leo June 26, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa onyo kali kwa watu wanaosafirisha chakula nje ya nchi bila kuwa na kibali akiwata wafanyabiashara hao kuzingatia hali ya chakula iliyopo nchini na kuchukua tahadhari.
Akihutubia kwenye Baraza la Eid Waziri Mkuu amesema:>>>”Tumezuia kutoa chakula sasa kupeleka nje ya Nchi kwa sababu uzalishaji huu hautoshelezi mahitaji ya Nchi. Nchi zote zinazotuzunguka jirani hazina chakula, hazikuwa na uzalishaji mzuri. Leo hii tuna maombi kutoka nchi jirani Somalia; Ethiopia, Sudan Kusini, Congo wametuandikia barua rasmi wakiomba kupewa msaada wa chakula wakati huku ndani na sisi hatuna chakula cha kutosha.
“Tunao wafanya biashara hao wanakimbiza chakula bila vibali. Naomba mnisikilize vizuri, kuanzia leo marufuku kwa yeyote kusafirisha chakula kwenda nje ya nchi bila ya vibali. Serikali imehamasisha kuwa na viwanda nchini na kama tutatoa vibali basi chakula hicho tutaanza kukisaga ili mupeleke unga na sio mahindi.
Aidha, Waziri Majaliwa amewataka wafanyabiashara hao kufuata taratibu za kupata kibali cha kusafirisha chakula nje ya nchi lakini watatakiwa kwanza kusaga mahindi na nje ya nchi upelekwe unga ili kulinda ajira nchini.
“Kama kweli unaona kuna umuhimu wa kupeleka chakula nje kwanza kaombe kibali na kibali hicho kitakuruhusu kusaga upeleke unga na sio mahindi. Ukipeleka mahindi kwanza unapunguza ajira ya nchi.” – Waziri Mkuu Majaliwa.
https://youtu.be/iP1rO7dXAbE
Baada ya JPM, Waziri Nchemba naye ametoa marufuku!!!