Moja ya story ambayo ina-make headlines kutoka Mwanza ni kuhusu uvamizi wa Kanisa la EAGT City Center la Mkuyuni Mwanza uliofanywa na kundi la watu saa 11 alfajir na kulibomoa.
Ayo TV na millardayo.com zimempata Mama Moses Kulola ambaye ni bibi yake Madam Flora na Mlezi wa Kanisa hilo na kueleza zaidi kisa cha kuvamiwa na kuvunjwa Kanisa hilo.
“Nimepigiwa simu tu kwamba wamevamia ukuta walinzi hapo mlangoni wakaanza kuwapiga na kuwaumiza. Wakaingia humu ndani na walipoingia wakaiba viti walipokimbia walinzi na mabati na maiki zote, Spika na ngoma za kwaya wamezibomoa.
“Hii ni nyumba ya Mungu. Najua heri ubomoe nyumba yangu mimi binafsi lakini nyumba ya Mungu ni jicho la Mungu. Hapa watu wanakwenda kuabudu na kuombewa, matatizo yao yanaondolewa na Mungu. Hapo atakayeshughulika na hao waliobomoa ni Mungu sio sisi.” – Mama Moses Kulola.
VIDEO hii hapa chini ina kila kitu…bonyeza PLAY kutazama ili kujua kila kitu!!!
Kutoka Makao Makuu ya TAKUKURU Rais wa TFF Malinzi na Katibu Mkuu wanashikiliwa!!!