Kazi ya Millard Ayo ni kukukusanyia na kukusogezea karibu stori zote kubwa na breaking news zote kutoka ndani na nje ya nchi ambapo leo July 2, 2017 yapo mengi yameripotiwa kwenye Televisheni, Radio, Magazeti na mitandao mbalimbali.
Kama ulikosa time ya kufuatilia habari moto moto Asubuhi hii ya siku ya pili ya mwezi July nimekukusanyia zote na kukuwekea karibu yako kupitia millardayo.com.
Serikali imetakia kukamilisha kwa wakati miradi ya maendeleo kwa Halmashauri zake ili kukabiliana na changamoto mbalimbali. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye amesema Serikali na viongozi mbalimbali walihusika kubeba na kuwakingia kifua watuhumiwa wa ESCROW #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Imeelezwa sheria zinazosimamia masuala ya mafuta, gesi ni dhaifu hali inayoweza kusababisha nchi kutofaidika kwa kiwango stahiki. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Serikali imeanza mkakati wa kupata mbinu mpya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya afya hasa magonjwa ya mlipuko. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Wakazi wawili wa Mharamba, Geita wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Sekondari ya Makoka, DSM amejiua kwa kujinyonga kwa kinachodaiwa kuliwa fedha za shule kwenye kamari. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka Serikali kutengua kauli yake ya katazo la wafanyabiashara kuuza mahindi nje ya nchi. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Jeshi la Polisi limemteua Kamishna Msaidizi wa Polisi Barnabas Mwakulukwa kuwa msemaji wake kuchukua nafasi ya Advera Bulimba. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa bandia na zilizo chini ya viwango zenye thamani ya Tsh. 2.4b. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
TAKUKURU imemfikisha Mahakamani mpima ramani msaidizi Manispaa ya Tabora akituhumiwa kujipatia Tsh. 16.2m kwa njia ya udanganyifu #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Serikali itaendelea kushirikiana na vyombo vya Habari kuhakikisha vinahusishwa katika masuala mbalimbali ya kuuhabarisha umma. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Imeelezwa kuwa miswada iliyowasilishwa Bungeni kwa ajili ya marekebisho haihusu madini pekee bali na kulinda rasilimali za nchi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Rais JPM ameahidi kuwa ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya Mto Ruvu (Stiegler's Gorge) lazima ufanyike. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
TAKUKURU Mkoa wa Geita imemfikisha Mahakamani aliyekuwa Afisa Ugavi Halmashauri ya Mji wa Geita kwa makosa 13 ya kughushi vyeti. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano haitomsamehe mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhirifu wa mali za ushirika #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Imeelezwa kuwa ongezeko la vijana mtaani wasiokuwa na ajira halisababishwi na ukosefu wa elimu, bali hawajui namna ya kujiajiri. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Mkazi mmoja wa Kalambo, Rukwa Adam Joseph (30) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mpwa wake akimdai gunia moja la alizeti. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Waziri katika Ofisi ya Rais Z'bar amekanusha madai kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetengwa kidiplomasia na nchi za Ulaya. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo na viungo wameilalamikia Serikali kushindwa kutatua changamoto zao. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Rais JPM ameitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) kuachana na mpango wa kujenga Hotel badala yake wajenge viwanda. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria alilazimika kusitisha kikao kulichojadili miswada ya sheria baada ya kuibuka mzozo. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Tukio la kupotea kwa Mtangazaji wa Azam TV, Fatna Ramole kisha kuonekana limezua utata, Polisi yasema hakutekwa wala hakutoweka. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Mtalii raia wa Italia Nico Valsesia ameweka rekodi ya Dunia baada ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia muda wa saa 26:54. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Madereva 21 wakiwemo WaTZ 18 wanaofanya kazi katika Kampuni ya malori ya mizigo ya Alistair wametekwa na Waasi wanaodaiwa wa DRC. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Mauaji ya raia Kibiti, Rufiji na Mkuranga, Pwani yamesababisha CCM kuchelewesha uchaguzi wake katika ngazi za shina hadi Wilaya. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 2, 2017
Serikali imewaagiza Wakuu wa Wilaya kote nchini kuwachukulia hatua kali watupa taka ovyo…hii VIDEO hapa chini ina kila kitu, bonyeza PLAY kutazama!!!
Siku kadhaa zilizopita Baraza la Wazee wa CHADEMA walizungumza mbele ya Waandishi wakitoa tamko kuhusu kauli ya Mzee Mwinyi lakini Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM wamewajibu wazee wa CHADEMA…bonyeza PLAY kwenye hii VIDEO kutazama!!!