Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini, Jumapili ya July 2 ilicheza mchezo wake wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana ambao ni wenyeji.
Tanzania ambayo ilikuwa Kundi A na timu za Mauritius, Angola na Malawi, ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kumaliza kinara wa Kundi A ikiwa na point tano sawa na Angola lakini ilifuzu kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Good news ikufikie kuwa Tanzania inafuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya COSAFA kwa kuifunga Afrika Kusini ambao ndio timu mwenyeji kwa goli 1-0, goli likifungwa na Elias Maguli dakika ya 17 ya mchezo, Maguli pia ndio amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa mechi.
E.Maguli amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mechi ya Tanzania vs Afrika Kusini FT (1-0) goli kafunga Maguli dakika ya 17 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/ZeYWrAPURk
— millard ayo (@millardayo) July 2, 2017
Afrika Kusini ambao ndio timu mwenyeji walikuwa wakiutawala mchezo zaidi ya Tanzania, kitu ambacho hakikuweza kuwasaidia kusawazisha goli pamoja na kuwa nyumbani, hadi dakika 90 zinamalizika Afrika Kusini walikuwa wanaongoza kwa upigaji wa kona 14 kwa 3 hiyo inaonesha ni kiasi gani walikuwa wanaishambulia zaidi Tanzania.
E.Maguli anaifungia TaifaStars goli la kwanza dakika ya17 vs A.Kusini katika mchezo wa robo fainali (1-0) #COSAFACup2017 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/oobcZB1b8t
— millard ayo (@millardayo) July 2, 2017
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1