Leo ni July 4, 2017 ambapo kama ulipitwa na story zote kubwa kwenye magazeti ya Tanzania asubuhi ya leo kupitia Televisheni, Radio, Magazeti au Mitandao mbalimbali ya kijamii nimekukusanyia na kukusogezea hapa kupitia millardayo.com.
Waandishi wa Habari na wadau wa sekta hiyo wamekumbushwa kufanyakazi kwa kuheshimu sheria, taratibu na maadili ili kulinda amani. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Serikali imeshauriwa kuanzisha ujenzi wa mitambo ya kuchakata na kuchenjua malighafi za rasilimali kuwezesha wavunaji kupata huduma. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Polisi Morogoro limekamata dawa zinazodhaniwa za kulevya aina ya bangi debe 2, 1kg ya heroine na meno mawili ya tembo yenye 15kg. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Serikali imewataka wananchi kununua bidhaa za ndani ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo kufikia lengo la uchumi wa kati. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Muda wowote kuanzia sasa zaidi ya nyumba 800 zilizojengwa ktk hifadhi ya barabara ya Morogoro zitabomolewa kupanua barabara hiyo. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Imeelezwa Mamlaka ya Mapato Tanzania imekusanya kodi ya majengo kwa ufanisi ukilinganisha na ilivyokuwa inafanywa na Halmashauri. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
TAKUKURU Mkoani Mara inamchunguza aliyekuwa mtumishi wa Idara ya Afya Joseph Baraka kwa tuhuma za ubadhilifu wa Tsh. 800,000. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
UVCCM imesema Waziri Mkuu wa zamani, Sumaye amekuwa anailaumu Serikali kwa kuwa hafahamu dhana ya demokrasia ya vyama vingi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM linadaiwa kumshikilia aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Mbunge wa Viti Maalumu, Juliana Shonza (CCM) amenusurika kupigwa na Wabunge wenzake wa upinzani akidaiwa kutoa lugha ya kuudhi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
"Mawazo yenu ni mazuri, naomba kwa sasa dhamira yetu iwe ni viwanda zaidi na si hoteli zaidi." – Rais Magufuli. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Mkazi wa Kambarage, Mwanza anayedaiwa kuwa mgonjwa wa akili anadaiwa kuwachoma moto watoto na wajukuu wake wakiwa wamelala usiku. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Polisi Morogoro inamshikilia mkazi wa Mlali kwa tuhuma za kukutwa na meno mawili ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Tsh. 33m. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Serikali imetangaza kuwa bado kuna idadi kubwa ya maofisa afya wakiwemo madaktari ambao wana vyeti feki. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema kitendo cha Rais Magufuli kuwataka wafunge midomo ni kuminya haki ya watu kutoa maoni yao. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Rais wa TFF Jamal Malinzi na wenzake wamerudishwa rumande baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukataa maombi ya dhamana. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Rais JPM yupo Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku 2 ambako atazindua mradi wa uboreshaji wa maji safi na usafi wa mazingira. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaongezea mashtaka 6 mmiliki wa IPTL Harbinder Seth na mfanyabiashara James Rugemarila. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
BAWACHA wamepinga Rais JPM kuweka zuio la wanafunzi wajawazito kutorudi shule wakisema ni kinyume na makubaliano ya kimataifa #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haikubaliani na Serikali kupeleka miswada ya dharura wakishangaa kutaka kupitishwa haraka. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Serikali imeombwa kupelekea umeme Kibiti ili kudhibiti mauaji ya raia ambayo yanafanyika kwa kuwa eneo hilo halina umeme. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Watanzania wametakiwa kutobaguana kwa itikadi za vyama, dini na kabila badala yake wadumishe umoja, upendo na mshikamano. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
Serikali imependekezwa kupeleka Bungeni muswada wa dharura ujadiliwe kuwa sheria itakayowaondolea kinga Marais wastaafu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 4, 2017
FULL VIDEO: JPM alivyotua Mwanza na kutembea kwa miguu hadi uwanja wa Nyamagana!!