Hivi karibuni kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitangazwa kutengwa kwa chumba maaum kwa ajili ya Wabunge wanawake wenye watoto wanaonyonya kukitumia chumba hicho kwa ajili ya kuwanyonyeshea watoto wao.
Sasa Sheria ya Tanzania ikoje kwenye mambo kama hayo? Mwanasheria Jebra Kambole amekaa na sisi kwenye Ayo TV na millardayo.com kutueleza…
“Ni suala kubwa sana kwa harakati za akina mama na watoto katika kutimiza wajibu wao kwa sababu tunategemea kwamba mama ndio msingi wa Taifa lolote…Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 12 inasema kila mtu ana wajibu wa kutunzwa heshima yake na kuheshimiwa.
“Tunaamini mtu anapokuwa ananyonyesha anahitaji kuwa na faragha, anahitaji kukaa sehemu nzuri lakini kwa kuwa hicho kitu kimefanyika mi nakipongeza na kinaenda sawa na Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungao wa Tanzania.
“Usiishie tu Bungeni pia katika Taasisi nyingine vitu kama hivi viwekwe ili watu wanaohusika na hayo mambo waweze kujihifadhi pale ambapo wanaamua kunyonyesha au wakati wanatimiza wajibu wao.” – Jebra Kambole.
DC Ally Hapi alivyoagiza kukamatwa kwa Mbunge Halima Mdee!!