Mahakama ya Delhi, India imemhukumu raia wa Tanzania ambaye alikamatwa na dawa za kulevya ikisema imefanya hivyo sio tu kwa sababu ya kujihusisha kwenye biashara hiyo bali pia ili iwe funzo kwake.
Katika taarifa iliyochapishwa na DNA (Daily News & Analysis) India, Ramadhan Ismail mwenye umri wa miaka 32 amekiri kosa akisema sababu ya kujiingiza kwenye biashara hiyo ni umasikini na majukumu ya katika familia.
Jaji maalum aliyeshughulikia kesi hiyo Sudesh Kumar alisema:>>>”Sababu kuu ya kumfunga mtuhumiwa siyo kufanya kosa pekee. Mahakama, wakati zinamuhukumu mtuhumiwa, lazima zijaribu, ndani ya sheria, kutoa nafasi kwa mtuhumiwa kujirekebisha na kumuongoza katika maisha ya kawaida, awe mtumishi wa jamii.” – Jaji Sudesh Kumar.
Adhabu hiyo imetolewa na Mahakama baada ya Ismail kupatikana na hatia ya kusafirisha 25kg za ephedrine ambapo alikamatwa na John Gugu, July 10, 2015, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi (IGIA).
Mtetezi wa Ismail, Anup Gupta alisema mtuhumiwa huyo alijiingiza kwenye kesi hiyo kutokana na umasikini akisema pia ni mgonjwa na amepoteza 38kg tangu alipokamatwa.
Anup Gupta aliieleza Mahakama kuwa:>>>”Familia yake inajumuisha mama yake, 56, bibi yake, 81, kaka zake watatu na dada yake. Hakuna mtu atakayewaangalia. Baba yake ameitelekeza familia muda mrefu.” – Gupta.
Mahakama imemhukumu kifungo cha muda alioutumikia na kulipa faini ya Rs 50,000, na akishindwa kufanya hivyo atatumikia kifungo rahisi cha mwezi mmoja.
VIDEO: Operesheni ya Dawa za Kulevya inavyoendelea na hatua iliyofikia hadi sasa!!!