Wizara ya Afya imetekeleza agizo la Rais JPM ambalo liliitaka Wizara ya Afya kuhakikisha Bohari ya Dawa ‘MSD’ inanunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji badala ya kununua kwa wauzaji au watu wa kati…
Good news ni kwamba Bohari ya Dawa ‘MSD’ imeanza kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji badala ya wauzaji na watu wa kati kama ilivyokuwa hapo awali huku miongoni mwa wazalishaji hao ni makampuni 10 ya Tanzania.
Waziri wa Afya Ummy Mwalim alisema:>>>”…wakati anafanya Kampeni aliahidi kuboresha upatikanaji wa dawa. Kwa hiyo dhamira yake hiyo sambamba na kuongeza Bajeti ya dawa aliniagiza kwamba tununue dawa kutoka moja kwa moja kwa wazalishaji, badala ya kununua dawa kutoka kwa Wafanyabiashara au watu wa kati.
“Na mimi hayakuwa maelekezo yangu, yalikuwa maelekezo ya Rais. Yalipita kwangu nikawapatia…Rais mwenyewe alirudia maelekezo yake kwamba anataka Wizara ya Afya kupitia MSD tununue dawa kutoka kwa wazalishaji moja kwa moja.” – Ummy Mwalim.
Mkurugenzi wa jiji DSM atozwa faini ya Tsh. 25m…ilipwe ndani ya siku 14!!!